Miili kama hii kwakweli ni hatari ukiona unakaribia au umefikia hapo jua uko
hatarini sana kwa magonjwa mengi na yahatari sana kwako.
Kama inavyojulikana mafuta mengi mwilini sio mazuri na asilimia kubwa ya watu duniani wana ugua magonjwa yanayosababishwa na kuwa na mafuta mengi mwilini,hizi ni baadhi ya njia kama mbili tuu za kupunguza body fats.
1.
Fanya mazoezi asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako.
Unapoamka asubuhi hakikisha unafanya mazoezi kwa muda usio pungua nusu saa au zaidi,Tafiti zinaonyesha kufanya mazoezi asubuhi kunasaidia kupunguza fat mara 3 zaidi ya muda mwingine wowote.
Na hii ni kwasababu mchana mzima mwili wako unapata nguvu(Energy) kupitia wanga(carbohydrates) ambao unaupata katika vyakula unavyokula siku nzima,Lakini unapolala usiku mwiliwako unatumia carbohydrates yote kama energy katika kazi mbalimbali za mwili zinazofanyika wakati umelala,
Kwahiyo wakati unaamka asubuhi mwili wako unakuwa hauna wanga (carbohydrates) kama energy yakutumia kwa wakati huo,
sasa kinachotokea hapa ni kwamba mwili wako utaunguza (burn) mafuta (Body fats) badala ya energy,Kwa maana hiyo basi ni vema ukafanya mazoezi asubuhi ili kuunguza mafuta ya mwilini vizuri zaidi,usinywe chai au kula kwanza kwani badala ya ku burn fats utakuwa unatumia carbohydrates ambayo umeipata baada ya kula kama chanzo cha nguvu kwahiyo huta unguza mafuta.
Na kitu kingine kizuri kufanya mazoezi asubuhi ni kwamba utafanya metabolism yako iwe fresh siku nzima na utajiskia ni mwenye furaha na umechangamka siku nzima,Na metabolism yako ikiwa fresh basi utaburn more calories kwahiyo utaloose weight vizuri sana.
2. Hakikisha unakunywa chai baada ya kumaliza mazoezi yako (workout)Hii ni njia nyingine yakufanya metabolism yako iwe fresh siku nzima,Baada ya kumaliza kufanya mazoezi asubuhi hakikisha unakunywa chai ili kuiwezesha body system yako kufanya kazi inavyo takiwa,Usiache kunywa chai mpaka mchana kwakuwa ukifanya hivyo mwili wako hautafanya kazi inavyotakiwa metabolism itakuwa slow kwahiyo huta weza kuburn extra fats mwilini,
Njia rahisi ya kuelewa ninachokisema ni hivi jaribu kufikiria kwamba mfumo wako wa mwili ni kama fireplace yani moto utaendelea kuwaka vizuri kama utakuwa unaweka kuni inavyotakiwa utaunguza mafuta mengi zaidi during the day kama kutakuwa na kitu tumboni kitakachofanya metabolism yako iendelee kufanya kazi kama kawaida wakati wote.Kwahiyo kunywa chai ni muhimu sana hasa baada ya mazoezi kwani kutakufanya uwe na nguvu siku nzima and inapunguza stress level.
ZINGATIABadala ya kula milo mingine miwili tuu kwa siku yani lunch and dinner,jaribu kula milo midogo midogo(small meals) minne(4) mpaka mitano(5) kwa nafasi ya masaa mawili(2) mpaka matatu(3) kwa siku nzima.kumbuka mfano wa fireplace niliyo kupa ,kwa kula hii milo midogo utakuwa kama unaweka kuni zinazotakiwa kufanya moto uwake vizuri yani your metabolism itakuwa inaburn more calories kwa siku mzima.Usi haribu mfumo wako wa chakula kwa kukaa na njaa halafu unakuja kula bonge la lunch au Dinner kwa kufanya hivyo utakuwa unakosea sana.
hakikisha metabolism yako inafanya kazi siku nzima bila kukosa kitu tumboni.
Wengi wetu tumekuwa tukikosea sana hapa unakuta mtu anafanya mazoezi sana halafu anasema mbona hapunguii???
Tatizo ni kutokujua kwetu kwamba kushinda na njaa ndio kupunguza mafuta kumbe sio kweli chakufanya ni kufanya mazoezi na ule vyakula vyenye afya na sio chips mayayi au vile vyenye mafuta mengi au sukari nyingi na pia kula kwenyewe kuwe ni kidogo kidogo kwa distance ya masaa 2 au matatu.sio mtu anashinda na njaa mchana kutwa then usiku anakuja kula bonge la chakula analala,hiyo haifai kabisa,
Na pia ukimaliza kula usiku hakikisha unakaa masaa mawili mpaka matatu kabla ya kuingia kulala ili kuwezesha chakula kusagwa kwanza.Jaribuni hili mtaniambia,Nasubiri mchango wenu.