Thursday, August 28, 2008

Mazoezi ya Kufanya Kwa Wale Wanaotaka Kumaliza Vitambi,Kutengeneza(six packs)

Ndugu zangu leo nataka kuelezea baadhi ya mazoezi ambayo yatakusaidia kukata Tumbo lako vizuri kama yatafanywa vema,ila kaa ukijua kwamba mazoezi haya pekee hayawezi kukupa matokeo mazuri kama hutashiriki mazoezi mengine ya kupunguza mafuta kama kukimbia,kuendesha baiskeli,kuogelea,kutembea haraka haraka,kucheza mpira na mengine mengi soma topic iliyopita,Mazoezi haya ni kwa ajili yakutengeneza masozi(muscles) za tumbo kuwa ngumu na kukupa shape nzuri(six packs),hata kama yanakata mafuta basi ni kwa asilimia ndogo sana kwahiyo usifanye haya mazoezi peke yake ukidhani kuwa ndio utapunguza tumbo hapana.

ONYO
Mazoezi ya tumbo ntakayoyaelezea yafanywe kwa umakini sana kwa watu ambao walisha wahi kufanyiwa upasuaji wowote wa tumbo ikiwa ni wanawake kwa uzazi au kwa matatizo mengine yoyote,kwani yanaweza kukuletea matatizo mengine makubwa zaidi.

Tumbo kama tumbo limegawanyika katika sehemu mbili:Tumbo la juu na Tumbo la chini,Katika mgawanyo huu kila sehemu ya tumbo inamazoezi yake ingawa yapo yale general kwa ajili ya tumbo zima.

katika picha huo ndio mwonekano halisi wa ninacho kisema katika kugawanyika kwa tumbo.

Mazoezi ya Tumbo la juu:
Kuna mazoezi tofauti na mengi ya kufanya kwa ajili ya tumbo la juu,hii inategemea ni vifaa gani ulivyo navyo kama ni GYM au nyumbani,mimi ntazungumzia mazoezi machache ambayo unaweza kufanya sio lazima uwe GYM hata nyumbani ili mradi upate kanafasi kidogo.
  • Lala na mgongo halafu miguu yako kunja itengeneze V shape huku viganyagio vikiwa chini,na mikono yako yote ikiwa nyuma ya kichwa chako,then nyanyua sehemu ya juu ya mwili(kichwa na mabega) kufwata magoti yako huku ukigeuka upande mmoja baada ya mwingine,fanya marudio mara 7 pumzika sekunde chache isizidi dakika halafu rudia tena mara 7 kwa round 3. angalia mfano huu..


  • Lala na mgongo kama tulivyoona zoezi la kwanza ila hili tofauti yake sasa badala ya kukunja miguu unakuwa umeinyoosha kama kawaida ila sasa wakati unanyanyua sehemu ya juu ya mwili unakunja na mguu mmoja kuufwata huku mwingine ukiwa umenyooka,mfano wake ni kama mtu ukiwa unaendesha baskeli unavyokunja miguu kwa kupishana,Rudia mara zile zile kama nilivyoeleza kwenye zoezi la kwanza. Angalia mfano huu...
  • Rudia kulala na mgongo miguu yako kunja kama tulivyofanya zoezi la kwanza ila sasa hili tofauti yake ni kwamba badala ya kunyanyua sehemu ya juu kidogo na kugeuka upande mmoja baada ya mwingine,hili una nyanyua sehemu ya juu ya mwili na kufwata magoti yako moja kwa moja,kwa wanao anza hili ni zoezi gumu kidogo inabidi uwe na mtu akushike miguu ili uweze kufanikiwa kulifanya au kama unamahali unaweza kuchomeka miguu ili kujizuia,lugha ya kigeni tunaita (Sit ups on floor) angalia mfano huu...
  • Zoezi hili pia unaweza kulifanya kama una bench lako zuri kwa ajili ya mazoezi ya tumbo au kama uko GYM zoezi hili ni zuri sana kama utaweza kulifanya kwani linagusa karibu matumbo yote la juu na lachini,kumbuka kufanya kwa round tatu na round moja fanya mara 7 na ukipumzika sio zaidi ya dakika moja kwa mara moja.angalia mfano...

Mazoezi ya tumbo la Chini:
Hili ndilo tumbo gumu kutoka kuliko maelezo na limekuwa likisumbua watu wengi sana,lakini ukilizingatia kwa mazoezi magumu kidogo kwani hakuna kitu kizuri kiraisi lazima usote kidogo linakwisha na utabaki na umbile lako zuri kama kawaida,(work hard for better Achievements)
  • Kama kawaida lala na mgongo na miguu yako yote uwe umenyoosha,mikono yako iwe nyuma ya makalio yako then nyanyua miguu yako nyuzi 90 na kuirudisha chini tena fanya hivyo kwa mara 7 na kupumzika sekunde chache na kurudia hivyo kwa mara tatu. hili ni zoezi zuri sana kwa tumbo utalisikia mapema sana tumbo likivuta,angalia mfanoo.....
  • Lala na mgongo tena na miguu yako nyoosha kama kawaida na mikono yako ikiwa nyuma ya kichwa chako halafu anza kukunja miguu yako yote miwili kuja usawa wa kifua chako na kuiinyoosha tena mpaka chini fanya hivyo kwa mara kadhaa kama nilivyo elekeza juu.
  • Ugumu wa zoezi hili ni kwamba kuna wakati unahitaji kuwa na mashine ya kukusaidi kulifanya hapa kuna faida kwa wale wanao fanyia GYM kwani naamini kuna vifaa vingi,mfano ni kama ukitaka kufanya zoezi hili hapo chini ambalo pia ni zoezi zuri sana kwa tumbo la chini.

Mwisho kabisa ni zoezi ambalo ni gumu kidogo kwa wale wanao anza ambalo mimi huwa nalipenda sana na huwa nalifanyaga karibu kila mara na lina matunda mazuri sana kama ukifanikiwa kuliweza vema,Nunua roller mashine yako kama hii..
na ujifunze kuitumia kama hivi...

Nashauri ukitaka kufanya zoezi hili basi uwe na mtu karibu akushikilie miguu na uanze taratibu taratibu wala usiwe na haraka utaweza na utakuwa unafanya mwenyewe hata bila kushikiliwa tena ,ni zoezi zuri sana kwa mwili mzima hasa sehemu ya juu ya mwili na tumbo lote kwa ujumla ukisha kuja kuzoea unaweza ukawa unafanya hili peke yake kwa siku kama zoezi la tumbo.

NB
Zingatia sana chakula unachokula usiache chakula kabisa bali epuka vyakula vyenye sukari (mfano soda,ice cream na hata kama ni mnywaji wa pombe basi yakupasa pia upunguze kwanza taratibu taratibu kwani BIA ndio mbaya sana kwa starch yake) nyingi na kama wee ni mnene sana tayari basi penda kula matunda na hata kama utakuwa unakula vyakula vya wanga kama wali,mihogo,ugali na viazi basi ule kwa kiwango kidogo zidisha zaidi mboga za majani na matunda kwa wingi,Pia usiku usipende kula vyakula vyenye wanga mwingi na hakikisha unakaa zaidi ya masaa mawili kabla ya kulala ili chakula kiwe kimesha fanyiwa kazi kabla ya kulala na usiache kula ila ule kidogo kidogo kwa distance ya masaa matatu mpaka manne na kama unafanya mazoezi ya kukimbia au mengine halafu ndio unakuja kumalizia na haya ya tumbo basi ni vizuri zaidi kwani utakuwa umeunguza calories vizuri sana mwilini.
Nasubiri nyongeza kutoka kwenu kwani tunaelimishana nami napaswa kujua kutoka kwenu.

5 comments:

Anonymous said...

Thanks kaka hii nimeipenda...mimi ni mtembeleaji wa blog hii almost kila siku..shule unayotoa ni nzuri sana kwa mtu anaezingatia...Gluv

BRAYAN said...

Asante sana kaka maoni yako na kuwepo kwako ndio kunatia moyo zaidi karibu sana tuboreshe afya zetu kwa pamoja.

Anonymous said...

asante sasa Byayan mimi ni yule mama niliyekuomba unipe shule ya mazoezi ya tumbo la chini ( manyama Uzembe) shule yako ni nzuri sana na sasa nimeanza mazoezi na nakunywa maji mengi sana na pia nakula mboga mboga na matunda kwa wingi na vyakula vya protein kama ulivyosema. pia nimeanza kukimbia ila naona nitaswim zaidi maana kama ulivyoshauri awali zoezi la kuogelez ni zuri zaidi.
pia usisahahu basi kuturushia zoezi la hips ni muhimu sana kaka yangu.

Asante na ubarikiwe sana katika kazi yako.

BRAYAN said...

asante sana mama yangu ucjali ntakuja na mambo mazuri kwa ajili yako wewe uwe unapita tuu uckate tamaa.......

Anonymous said...

LEO NDIO NIMEISOMA NIMEIPENDA ILA NAAANZA KIFANYA MAZOEZI ILI NIONE MATOKEO USISAHAU KUONDOA HIPS MAANA TUNAZO BALLA