Tuesday, August 26, 2008

Vitu vya kuzingatia kwa wanao anza mazoezi ya kupunguza uzito(mafuta mwilini (VITAMBI) ) kwa mara ya kwanza.

Wadau leo ningependa kugusia mambo muhimu kwa wale wanao anza mazoezi kwa mara ya kwanza (beginners) ni nini chakufanya ili wasikate tamaa na kuacha kabla ya lengo na pili wasiumize mwili na kushindwa kuendelea tena kwa siku zinazofuata,kwani mwili wa mwanadamu unahitaji mapumziko yakutosha ili kuweza kuwa na akili na afya njema kwa ujumla.



Kabla sijasema mambo hayo ningependa niwashirikishe kitu kidogo ingawa kiko katika lugha ya kigeni lakini natumaini wengi tunaelewa kama itasumbua basi usisite kusema kwa msaada....

Staying Commited
As in everything we do in our lives. , when it comes to staying healthy and being fit, COMMITMENT is where it starts and finishes. Now more than ever, it is important to stay committed because those who are stressful in reaching their goals and maintaining the body they want are the people who
  1. Can always visualize their goals clearly,
  2. Have inner strength, and determination to archives their goals.

Baada ya kidokezo hicho tuje sasa kuangalia mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kuanza mazoezi:
  1. Jiulize ni kwanini unataka kufanya mazoezi?
  2. Panga muda wako mzuri ili usigongane na shuguli nyingine muhimu za kimaisha.(Asubuhi na mapema Recommended)
  3. Hakikisha mwili wako ni mzima kiafya(huna maleria na magojwa mengine yakawaida)
  4. Tengeneza ratiba yako ya mazoezi,(siku ngapi na ni mazoezi gani utafanya)
  5. Kuwa na malengo(baada ya mwezi mmoja nataka niwe nimepungua kilo 2 mfano)
  6. Hakikisha unapima kilo zako kabla ya kuanza mazoezi(hukutia moyo ukijua umepungua)
  7. Anza kidogo kidogo(yani inaweza kuwa mara 3 au 4 kwa wiki ila iwe ni zaidi ya 30 mnts)
  8. Pata muda wa kupumzika vyakutosha.
Ningependa kushauri kwamba kwa wale wote ambao ndio mara ya kwanza wanaanza mazoezi ya kupungua kwa mwezi wote wa kwanza wafanye mazoezi ya kukimbia tuu na kunyoosha viungo(ingawa zoezi sio kukimbia tuu hata kuogelea ni zoezi kubwa sana nafikiri ndio zoezi number moja duniani linalopunguza uzito haraka zaidi kuliko mengine kwa mujibu wa wachunguzi) ili kuupa mwili taharifa ya nini kinakuja au kuaandaa mwili kwa lugha nyingine wakati huo pia unatengeneza na pumzi yakukusaidia katika mazoezi yanayofuata baada ya hapo.

Unajua kwanini napendelea kukimbia?? its because
Running is a free, simple, and healthy outlet for stress.


Angalia list hiyo hapo chini ilivyo onyesha mazoezi mbalimbali na jinsi yanavyo burn calories:


Nasubiri mawazo kutoka kwenu wadau wangu,ningependa kama baada ya wiki nipate majibu kwamba wadau kibao wanafanikisha hili.

5 comments:

Unknown said...

Nice blog Brayan!

Anonymous said...

safi kaka brayan ila rangi ya hayoo maandishi hainoshi vizuri sisi wabovu wa macho

Anonymous said...

Mimi ni mvulana wa miaka 27.Jamani mie ni mnene kiasi ambao ni wa kawaida tu na wengi wanao..ila nina kitambi sijui kimetoka wapi..sipendi.nimekuwa nikifanya mazoezi na kuacha kula wakati mwingine japo nakuwa weak sana ila kitambi bado kipo..nakuwa nipo fiti na afya lakini kitambi kimeniganda..sinywi pombe kabisa..sasa nifanyeje ..je ni vyakula????naomba njia rahisi na ya muda mfupi na natural ..

Anonymous said...

habari kaka Brayan. ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye blog yako but nafikiri sija miss sana.

jambo la kwanza kiushauri naomba ubadilishe appearence ya blog yako ili wabovu wa macho (mimi mmoja wapo ) tuweze kusoma vizuri maana unatoa mafundisho mazuri sana naomba nikupongeze kwa hilo

pili mimi ni msichana na nina watoto tayari na ninatatizo moja nimekuwa na manyama uzembe sehemu ya tumbo la chini ambayo yamezunguka mpaka pembeni ya tumbo
pia sina hips so u can imagine the shape i am in

naomba msaada wako na nitashukuru kama utaweza kunishauri aina gani ya mazoezi natakiwa kufanya ili niondokane na manyama uzembe na aina gani ya mazoezi ili niweze kuwa na hips na aina gani ya chakula cha kula na aina gani ya chakula cha kuavoid.

nitashukuru sana kwa msaada wako ambao najua utawasaidia wanawake wengine ambao wanatatizo kama langu

BRAYAN said...

Dada yangu na Kaka yangu natumaini ntakuwa nimewajibu kidogo maswali yenu kuhusu mazoezi ya tumbo na chakula ebu jaribuni kwanza kupitia topic hiyo mpya halafu kama bado kunatatizo mtaniandikia tena wala msisite karibuni sana.