Thursday, September 11, 2008

Sitaki kupungua mwili ila nataka kutoa kitambi peke yake je nifanyeje?

Nimepata maswali mengi sana kutoka kwa watu mbalimbali kuhusiana na swala la kupungua sehemu moja tuu ya mwili na hasa kutoa kitambi peke yake bila kupungua mwili mzima,nimeamua kujibu hapa ili kuwapa faida wasomaji wangu wengine.

Kwanza kabisa tujue kwamba kuwa na kitambi na kuwa na mafuta(FATS) mengi mwilini ni vitu vinavyo endana kwa ukaribu sana kwani Fats nyingi mwilini hufanya storage kwenye tumbo na hata kwenda kwenye makalio(matako) hii ni kwa wanaume,na kwa wanawake fat storage hufanyika kwenye misuli ya mikono ya nyuma(triceps),hips,matakoni na baadaye kuhamia kwenye tumbo,


Tafiti zinasema kuwa fats zinazokuwa tumboni ndio fats mbaya kuliko fats nyingine zote ambazo ziko mwilini,inasemekana kuwa ndio fats zinazosababisha higher cholesterol levels,higher blood sugar,heart disease and raised blood pressure.

Kwahiyo sasa unapotaka kupungua jua kuwa unataka kutoa mafuta mwilini kwahiyo ili utoe mafuta ni lazima ufanye mazoezi ambayo yatatoa Fats ndani ya mwili mzima na sio sehemu moja tuu ya mwili,Unaweza ukafanya sana situps na mazoezi mengine mengi ya tumbo lakini tumbo halitapungua bali utalikomaza tuu na mwishoni litakuwa gumu zaidi hata kutoa fats zilizomo.

Ningependa kuwaambia wasomaji wangu kwamba hakuna zoezi la kutoa kitambi peke yake bila kupungua mwili mzima na ni ngumu sana kutoa body Fats kama hutafanya mazoezi ya kushirikisha mwili wako wote kwa muda wa lisaa limoja au dakika 45,kwa kawaida mwili huanza kuburn Body Fats kwa ajili ya kutumika kama enegry baada ya nusu saa wakati unafanya zoezi.

Kabla ya hapo mwili unakuwa unatumia the available energy, kwa mfano wakati ukiwa unakimbia au kuendesha baiskeli baada ya nusu saa mwili wako huanza kuunguza mafuta kwa ajili ya kukupa nguvu ya wewe kuendelea na ndipo hapo tunasema unaburn calories mwilini.

Ushauri wangu kwa wasomaji wangu ni kwamba njia pekee ya kupungua ni kufanya mazoezi yanayo shirikisha viungo vyako vyote kwa pamoja na hakikisha unafanya kwa muda usio pungua lisaa limoja au dakika 45.
Na kama unamwili wa kawaida hutaki kupungua bali unapenda kufanya mazoezi kwa ajili ya afya basi fanya mazoezi kwa nusu saa tuu kwa wiki hata mara tatu sio mbaya utaendelea kuonekana ni mwenye afya na mtanashati na unae jiamini kwa wakati wote.
Nasubiri maoni na mchango wenu asanteni pia kwa kuwa wasomaji wangu wazuri.

6 comments:

Anonymous said...

Hi Brian,

i like your blog sana tu, na nina swali nataka kujua je CD za mazoezi for beginners zipo na je zinauzwaje? mimi nataka kupungua mwili mzima ila sitaki kukimbia nataka kufanya mazoezi ya kawaida tu kama vipe aerobics etc.

nisaidie kwa hilo

Anonymous said...

Hi Brian,

i like your blog sana tu, na nina swali nataka kujua je CD za mazoezi for beginners zipo na je zinauzwaje? mimi nataka kupungua mwili mzima ila sitaki kukimbia nataka kufanya mazoezi ya kawaida tu kama vipe aerobics etc.

nisaidie kwa hilo

Anonymous said...

Asante kaka kwa darasa lako..nimekupata!!sasa naomba ushauri wako katika mpango wangu huu sasa wa kutoa hiki kitambi..
Nataka nifanye mazoezi ya kutosha na kupunguza kula sana/ovyo na kufuata mpangilio wako wa mazoezi ya kupunguza mwili....Kisha nataka kurudi kwenye unene wangu huu yaani mwili mkubwa ila sitaki kitambi kirudi maana nitakuwa nakula sana kama kawa.
Gluv Jr

BRAYAN said...

Asante sana kwa kuwa mtembeleaji mzuri wa mahali hapa,
kwa sasa sina CD ila baadae zitakuwepo kwahiyo ucjali ila ntakupa mazoezi ya kufanya kwa sasa ili usiboreke sana kwa kipindi hiki,ndio naandaa topic nzuri kwa ajili yenu,
aerobics ni mazoezi mazuri sana hasa kama nyumba yako inanafasi basi ni vema ukafanya asubuhi.kama una swali lingine au tatizo plz dont hesitate my email is
brayanmawela@gmail.com.

Anonymous said...

Hi Brayan,

nakupongeza kwa kazi nzuri ya kutuelimisha sisi tuliokuwa hatujui faida ya mazoezi. mimi ninatatizo moja kaka, nimejifungua kwa operation sasa mwanzo nilipungua vizuri lakni tokana na mtoto kunyonya sana nimenenepa sana mpaka najichukia na sasa mtoto ana mwaka na nusu. mazoezi gani yanafaa kwa waliozaa kwa operation. siku njema

Anonymous said...

hey Bryan.... mwili wangu ni kawada tu ila naona kama dalili ya kitambi kinatoka coz nai feel kwa mbali wa na watu washaanza kunisema....
Joe