Thursday, August 21, 2008

Vyakula Vyakuzingatia wakati ukiwa unafanya mazoezi ya kupunguza mafuta mwilini.


Vyakula ni muhimu sana hasa wakati mtu unataka kupungua vema na kuwa na afya,maana walio wengi wana amini unene ndio afya kumbe si kweli. Ni vizuri ukawa na ratiba ya vyakula vya kuzingatia na kujua pia faida zake mwilini sio kula tu ilimradi umekula.Kuna aina mbalimbali ya makundi ya chakula nayo ni kama
  1. Wanga (Carbohydrates).
  2. Protein.
  3. Mafuta (fats and oils).
  4. Vitamini (vitamins).
Carbohydrates ni aina ya chakula ambacho ndani yake kina carbon,Hydrogen na oxygen pia kuna sukari na wanga ndani yake (starches) ambavyo hutumika mwilini kutengeneza nguvu(to produce energy) ,Carbohydrates kwa kawaida hupatikana kwenye mimea (plant Sources). Carbohydrates ikiingia mwilini huvunjwavujwa na kutengeneza glucose ambayo ndio hutumika kuupa mwili nguvu. Nguvu mwilini hutumika katika makundi mawili ambayo ni Ndani ya mwili na Nje ya mwili
  • Ndani ya mwili ni kama Kupumua,Kusukuma damu,Kusaga chakula na kazi nyingine za mwilini.
  • Nje ya mwili ni kama Kufanya kazi,Kucheza michezo mbalimbali na shughuli zozote zinazohusiha viungo vyako.
Na carbohydrates hii tunaipata kwenye mimea kama,
  1. Mboga za majani na matunda
  2. Sukari
  3. Mchele
  4. Ugali na vingine vya mfano wa mimea
  5. Spageti
  6. Mkate
Protein ina mchanganyiko wa carbon,oxygen,hydrogen and nitrogen,pia protein ina mchanganyiko mkubwa wa Amino acids. Protein hutumiwa na mwilini kufanya kazi zifwatazo
  • Kusaidia ukuaji na maendeleo ya kila siku ya mwili katika kuujenga.
  • Kutengeneza body structures kama muscles,tissues na organs including moyo,mapafu,na organs za kusaga chakula.
  • Kutengeneza Enzymes,kwa mfano zile zinazosaidia kusaga chakula.
  • Na hormones mbalimbali mwilini.
Kwahiyo ukiangalia utagundua kwamba protein ni muhimu sana mwilini na inaitajika na mwili sana.kwakuwa husaidia kusaga chakula na hata kukuza mwili wako. NB Watoto wadogo wanahitaji sana protein kuliko kitu kingine kwakuwa huwasaidia katika kukua kwao. Protein hupatikana katika vyakula kama,
  1. Nyama (meat)
  2. Samaki (Fish)
  3. Mayai (Eggs)
  4. Karanga na Maharage.
Mafuta(Fats and oils) ni chakula muhimu sana kwani mwili unahitaji fat kila siku kwa afya na kujisikia vizuri kama unavyohitaji vyakula vingine.
Fats inatumika mwilini kwa mambo mengi muhimu kama:
  • Katika muundo wa chembechembe hai za mwili (cell structure)
  • Kutengeneza nerves na akili.(the brain is 40% fat)
  • Kuupa mwili joto
  • Kutengeneza sex hormones
  • Kunyonya baadhi ya vitamini kama A,D,E and K

Mafuta (fats and oils) hupatikana kwenye..
  1. Animal meat
  2. Fish
  3. Vegetable oil
  4. Parachichi
  5. Njugu

Vitamins na Minerals ni vitu ambavyo vinapatikana katika aina mbalimbali ya vyakula,kwahiyo kwa kula vyakula tofauti unaweza kupata vitamins nyingi na minerals za kutosha kwa afya.
Minerals zinafanya mambo mengi sana mwilini ikiwemo kujenga mifupa na meno,kurekebisha mapigo ya moyo na kusafirisha oxygen kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye tissues.


Kwakula matunda kama haya na maziwa basi utakuwa umeupa mwili wako vitamins na minerals nyingi na zakutosha kwa afya yako.


NB
Katika makundi yote haya ya chakula niliyo yataja ni muhimu sana kuzingatia na kuhakikisha unapata kila kundi katika mlo wako wa siku,na pia ni vema kuzingatia kiwango unachokula kama nilivyosema katika topic iliyo pita kwamba usipendelee kula sana mpaka usikie tumbo limejaa,bali kula kidogo kidogo kwa nafasi ya masaa mawili mpaka matatu.Pili uzingatie maji yakutosha mwilini penda kujizoesha kunywa maji mara kwa mara na usipende kunywa maji mara tuu baada ya kumaliza kula kwani wataalamu wanasema kwamba maji baridi yanapokwenda tumboni system ya tumbo huanza kuyapooza kwanza maji ili yawe katika joto linalotakiwa kwa ajili ya kuingia kwenye system ya mwili,kwa wakati huo chakula kinakuwa kimesubirishwa kwanza kitu ambacho hakishauriwi kiafya.


Jaribu kubalance vyakula vyako kama jamaa hapo juu.


Mwisho kabisa ni kuzingatia mazoezi kila asubuhi,najua itakuwa ngumu kwa wanaoanza mara ya kwanza,Ntakuja na topic kuhusu jinsi ya kuanza mara ya kwanza mazoezi( Beginners)
Maana usingizi wa asubuhi si mchezo kama huna malengo inakuwa kazi kweli kweli....

6 comments:

KKMie said...

Unakuja sio hahahaha poua.

Nimefurahi kuona kitu kipya(kibongo bongo) na tofauti badala ya kuchukua "idea" ya mtu mwingine na kuandika mambo yale yale.

Hii itasaidia sana wanawake na wanaume kuwa na afya njema nje na ndani ya mwili na vilevile kuboresha matamaniano ya kimwili(mambo ya D'hicous) ambayo mazezi yana nafasi kubwa ktk kufanikisha hilo.

Nasubiri blogs za wajuzi wa (Sheria za kibongo), Afya ya akili, malezi ya watoto (tangu mimba).

Nimefurahi sana kukutana na kona hii. Endeleza kazi uliyoianza bila kusita.

BRAYAN said...

Karibu sana Dinah hope tupo pamoja katika kuijenga jamii yetu hii kiafya na kimaadili pia,Nakubali sana kazi zako since then so natumaini tutajenge kwa pamoja jamii yenye nguvu na kujiamini katika maisha yao ya kila siku kwani afya njema,maisha ya kimapenzi na upendo huumpa mtu kujiamini na furaha ya daima.

FJ said...

nimependa blog sana.. wazi... FJ

BRAYAN said...

Karibu sana Rose kuna mambo mengi mazuri yanakuja so uwe unapitapita uwaambie na mashoga zako pia kuwa vitambi sio dili tena nowadays hahahahahaa.

Anonymous said...

Kwakweli kazi nzuri huwa haijifichi,from nowhere utaona watu wana'notice uwepo wako na uwakilishaji wa kazi zako za maana,good work Kijana and keep it up.
Binafsi nimeanza mazoezi rasmi leo,nilitega saa 5:30am nikaamka,nikapiga zangu zoezi la kama 20mns hv(la kukimbia) then nikarudi kujiandaa kwaajili ya kuwahi mzigoni,nilishawahi kuwa na program ya aina hii lkn ilinishinda ku'maintain,lkn nimepania this time I should do something to strengthen my afya,cause haka kakitambi kanakoninyemelea kanaweza kuniletea problem mbele ya safari kama nitakaendekeza(kwani hata Shemeji yako ameshaanza kukilalamikia).
Naomba tu Mzee usiache kuja na mambo constructive kwaajili ya kutusaidia watu kama sisi.
By the way kwanini unapokuja na mada zako usi'feature na aina mbalimbali za mazoezi yanayotakiwa kufanywa na mtu anayetaka kuboresha afya yake,kwani wengi wetu kwa kukosa nafasi ya kuingia Gym tumeendelea kuwa mambumbu wa mazoezi,wengi wetu tunajua kukimbia tu yet kuna mazoezi ya aina nyingi tu ambayo yanaweza kumsaidia mtu kufikia malengo yake kwa haraka zaidi,kwa mfano nasikia kuna mazoezi hadi ya kukata tumbo,lkn yanakwendaje ndo hapo akina yakhe kama sisi tungependa tufahamu.
Anyway kwa leo naomba niachie hapa,ni hayo tu Mkubwa

BRAYAN said...

Ebwana anselm usijali kabisa mzee tupo pamoja nawaandalia topic nzuri sana kuhusu ni mazoezi gani unatakiwa kufanya so wewe kuwa karibu utapata kitu fresh,
ila kwa sasa nakupongeza sana kwa kuanza mazoezi na nimekupa tips hapo juu kwenye topic mpya so tuwe pamoja wewe zingatia ratiba yako tuu na mambo muhimu niliyo yataja.