Friday, September 5, 2008

Mazoezi ni raha sana hasa kwa muonekano wa mwili wako.

Ivi unajiskiaje unaposimama na kujiangalia kwenye kioo chumbani kwako ukiwa umetoka kuoga na kuona una mwili mkubwa na haujapangika hata kidogo nyama zimelegea tumbo kubwa (kitambi).Dada zetu hata kama ni hips basi zipo tuu lakini hazieleweki yani kwa ujumla mwili haukuvutii hata wewe binafsi ukijiangalia.Ni wengi sana wanatamani kuwa na miili mizuri na yenye mwonekano wenye afya na kupendeza kama baadhi ya mastaa wakubwa duniani lakini kinachowashinda ni uvivu na kutokujua ni nini mtu unataka na kwanini unataka.Katika maisha ni lazima mtu ujifunze kuishi kwa mipango na kuwa committed yote yatawezekana.

hebu angalia miili kama hii...


Ngoja niwaambieni kitu mwili wa binadamu na akili kwa ujumla unahitaji mazoea tuu na ukishajizoesha kufanya exercise mwili unazoea na siku ukikosa utahisi kama umepungukiwa na kitu kikubwa sana mwilini kwa ajili ya mazoezi na kweli ukiwa committed mazoezi hayadanganyi bwana yani mwili unakuwa na afya ngozi inakuwa safi huna hata haja ya kutumia vipodozi wewe ni mwendo wa rays tuu na unang’aa kama kawaida na utajiona ni mwenye furaha na kujiamini kila wakati.Jaribu leo utaniambia baada ya mwezi mmoja tuu na usikate tamaa kwani matunda ni taratibu taratibu tuu.

SWALI LA KIZUSHI KWANINI DADA ZETU WANAPENDA SANA WANAUME WENYE MIILI YA MAZOEZI(muscular guys) KAMA HII…..?????

4 comments:

Anonymous said...

Ni kweli binafsi napenda kuonekan kijana maridadi, sifagilii sana misuli naomba utupe mambo ya mazoezi ya kuunguza mafuta na misuli ya ziada rafiki. Kazi nzuri endelea kujitahidi wadau tupo

Anonymous said...

Sitaki kupungua mwili ila nataka kuoa kitambi peke yake je nifanyeje?..Gluv Jr...asante!

bizzy said...

kaka bryan vitu vyako navikubali, naomba kuulizahivi kuruka kamba inaweza kuwa ni zoezi tosha kuweza kuunguza mafuta yasiyohitajika mwilini na hatimaye kuondoa kitambi a.k.a manyama uzembe?

Anonymous said...

najiskia fresh kuwa na man aliyejengeka i hate kitambi